Kuhusu sisi
Historia yetu
Onfon Mobile ilianzishwa mwaka 2022 kama tawi la Onfon Group. Kampuni ilianzishwa kwa dhumuni la kutoa mikopo ya simu janja kwa gharama nafuu nchini Tanzania. Makao makuu ya kampuni yanapatikana jijini Nairobi, nchini Kenya, na dhima kuu ni kusimamia matawi yote yaliyopo Afrika Mashariki na Afrika ya Kati. Kampuni ina matawi jijini Dar es salaam, Tanzania na Kampala, nchini Uganda yanayowezesha kutoa huduma katika soko la Afrika Mashariki. Hata hivyo, kampuni ina matawi mengine yaliyopo jijini Lagos, Nigeria kwa ajili ya kuhudumia watu wa Afrika Magharibi pamoja na tawi lililopo Maputo, Mozambique kwa aajili ya kutoa huduma kusini mwa Afrika.
Maono
Kampuni ina maono ya kuiunganisha Afrika pamoja na kuboresha mazingira ya kidijitali barani hapa kwa kutoa simu janja zenye gharama nafuu.
Malengo
Kampuni inalenga kukuza teknolojia katika soko la Afrika kwa kuwapatia waafrika wengi fursa ya kumiliki simu janja kwa gharama nafuu.
Kwa nini uchague Onfon Mobile?
Nafuu
Chagua simu za aina mbalimbali, muda wowote. Hakuna nyongeza ya kodi.
Uhuru wa Kuchagua Malipo
Unaweza kulipia simu yako kwa muda wa miezi 12, ambapo unaweza kulipia kwa siku au zaidi kulingana na uchaguzi wako kwa mwaka mzima.
Uwazi
Malipo yote yanaonekana katika Aplikesheni yetu. Pindi mkopo wako utakapomalizika malipo ya simu yako yatasitishwa.
Rahisi
Huduma zetu zote zinapatikana kwa kutumia USSD piga *147*04# au kwa kutumia aplikesheni yetu ya Onfon Mobile.